Wednesday, September 21, 2011

USIACHE MBACHAO

BY ALI MWERO

Dawa ya moto ni moto ! Hapana , mvumilivu hula mbivu, naam lakini nimechoka. La! Siachi mbachao kwa msala upitao. Visa vilivyohadithiwa na hata kushuhudiwa katika chuo chetu kikuu cha moi. Visa vya wanagenzi kuvamiwa na almaarufu Mashoka na hataukosefu wa umeme ni mambo yaliyowakinai wengi na kutowapa usingizi.

Uvumilivu umewashinda na hatimaye wanaoishi jumba la H walijaribu kuzitoa hisia zao na mambo hayakwenda mrama. Wakubwa waliungama na hatimaye umeme si ndoto tena kwao. Katika jumba la J ninayo huruma belele kuhusu nmadada hawa. Katika katiba yetu ya Kenya imempendekeza mwanamke na kumpa hadhi si haba na pia kumjalia kipau mbele katika nnyanja tofauti tofauti. Lakini katika chuo chetu ni ndoto kwa madada wetu, kwani wameacha kwenye giza totoro. Hili ni jambo la kushangaza sana na ningeomba jambo hili liangaliwe kwa makini.

Si hayo tu, majumba mengine pia wanazisimulia shida hizi na nyingine kila uchao. Haya yalijiri takribani majuma matatu yaliyopita ambapo wengi walikuwa wamekereka si haba. Wengi walikosa mlo jioni ifikapo kwa sababu ya shughuli za masomo.

Mawazo mengi yamenijia akilini mwangu. Mwamburi wa mwang’ombe na baraza lake w anao uwezo wa kuchukua hatua mwafaka ili kuzitatua shida hizi kabila ya mambo kuingia nyongo na kubakia midomo wazi. Wanasema mkunje samaki angali mbichi. Mwamuri na baraza lako hamjachelewa kamwe na hamna budi kuwaeleza wanagenzi wengine kinaga ubaga ili kupata suluhu.

Bwana mwenyekiti shida haziishi lakini zinaweza kupunguzwa iwapo zitatatuliwa. Uko huru kama nikuonavyo. Umemshinda rais wa jamhuri yetu ya Kenya anayelindwa na askari wasiopunguamia tano. Lakini wewe umejiamini na ulinzi wowote, kongole! Kwa kifupi unazo njia nyingi za kutatua shida hizi.

Bwana mwenyekiti ulapo na kipofu usimuguse mkono, mbona wa mgusa mkono? Wamjulisha kuwa wamnyima haki yake . Comrades power! Comrades power! Ni maneno ambayo ushayasikia na kuyashuhudia wewe mwenyewe . kama maneno haya yanakukata maini kwa nini usiitishe mkutano na kuwaeleza ili wapate kukuelewa na waridhike.

Ninakusihi wewe mwenyekiti na baraza lako make kitako, mjadiliane kwa kina ili muweze kuibuka na suluhu la kudumu kuhusu shida zinazo kikumba chuo chetu maarufu. Ni jukumu lenu kuzivizia shida hizi na kuhakakisha hali ya usalama, umeme na mengimeyo ambayo hayajitokeza yanasuluhishwa barabara.l namuomba mola awape owezo wa kuleta mawazo yenu pamoja ili shida hizi zisilete mtafaruku.

Naam, kwa sisi akina yakhe tuliochoka kuvumilia na kutupilia msemo wambao mvumilivu hula mbivu nawasihi tuweni na subira kwani subira huvuta kheri. Kwa baraza la wanafunzi chini ya mwenyekiti, Bwana Mwamburi hamja kawia kumbukeni majuto ni mjukuu. Naam usiache mbachao kwa msala upitao.

No comments:

Post a Comment

your comment, your voice...

Search site.